Monday, February 1, 2016

JIJI LA DAR ES SALAAM LAPOKEA UGENI MZITO.

 
Dar es Salaam ina ugeni wa maktaba inayoelea majini
Wapo wanaoiita maktaba inayoelea. Maktaba hiyo ni pekee iliyowahi kuwafikia watu zaidi ya 44 milioni duniani tangu ilipoanza kuelea baharini miaka 40 iliyopita.
Hii ni meli kubwa ya kuuzia vitabu yenye jina la MV Logos Hope, ambayo kwa mara ya kwanza imetia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

WAZIRI ATOA TAMKO KALI KWA WAAJIRI.







 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki moja kwa waajiri nchini kuwapa mikataba ya ajira vibarua wao.Waziri huyo ametoa kauli hiyo alipokuwa akikakugua kituo cha Chiko ujenzi wa barabara Dodoma-Arusha unapoendelea,alitoa masaa 12 kwa vibarua wa kampuni hiyo ya ujenzi kuajiriwa.